Header Ads Widget

SIRRO ATOA NENO KUHUSU USALAMA KIGOMA

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka viongozi na wananchi wa mkoa Kigoma kuchukua tahadhari wakati wote kuhakikisha mkoa huo unakuwa salama dhidi ya vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha Amani ya mkoa huo.

Sirro alisema hayo akuzungumza na viongozi wa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu akieleza kuwa uchaguzi umekwisha na wananchi wote wanapaswa kuendelea na shughuli zao za kawaida lakini bado suala la ulinzi na Amani wa nchi lazima lipewe kipaumbele wakati wote.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa Mkoa Kigoma haukukumbwa na matukio ya vurugu kama yalivyotokea kwenye miji mikubwa nchini Zaidi ya rabsha ndogo ndogo za taratibu za uchaguzi ambazo zilipatiwa suluhu na uchaguzi kufanyika kwa Amani hadi kutangazwa kwa matokeo.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Abdallah Bukuku ameshukuru jeshi la polisi mkoani humo ambalo lilifanya kazi kubwa ya kusimamia ulinzi na usalama wakati wote wa kampeni na uchaguzi na wanaamini uchaguzI ulifanyika vizuri japokuwa kulikuwa na dosari ndogo ndogo.

Kwa upande wake Kiongozi wa Kimila wa Kabila la Waha wa mkoa Kigoma, Chief Alfred Kimenyi ameshukuru Mkuu wa mkoa Kigoma kuitisha Mkutano huo kuzungumza na kufanya tathmini ya uchaguzi nay ale yaliyotokea na kupongeza mkoa Kigoma kwa kuchukua tahadhari na hivyo mkoa kubaki salama wakati wote.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI