TAARIFA KWA UMMA
MAAZIMIO YA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM YA TAIFA KILICHOFANYΙΚΑ JIJINI DODOMA TAREHE 5 NOVEMBA 2025
Kikao maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kimefanyika leo tarehe 05.11.2025, jijini Dodoma. Hiki ni kikao cha kwanza kufanyika tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 hapa nchini.
Pamoja na mambo mengine, kikao hicho maalumu kilitafakari hali ya kisiasa nchini kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29/10/2025, na kuazimia kama ifuatavyo:-
i) Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa inawapongeza kwa dhati wananchi wote wa Tanzania kwa kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura na kuonesha imani kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
ii) Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa inalaani vitendo vya kihuni na uvunjifu wa amani vilivyofanywa na baadhi ya watu, vilivyosababisha vifo na uharibifu wa mali za umma na za wananchi.
iii) Chama Cha Mapinduzi kinaazimia kujitathimini na kujipanga vyema kubeba dhima ya kuliongoza Taifa.
iv) Chama Cha Mapinduzi kinaitaka Serikali kuchukua hatua muafaka za kuhakikisha nchi inabaki katika hali ya amani na utulivu.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Kenani Laban Kihongosi
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC)
Itikadi, Uenezi na Mafunzo






0 Comments