Na Ashrack Miraji Matukio Daima App
Singida. Mbunge wa Jimbo la Ilongero mkoani Singida, Haidarali Gulamali, amejisajili tayari kwa ajili ya kushiriki vikao vya Bunge la 13 vinavyotarajiwa kuanza rasmi Novemba 11, 2025, katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma. Usajili huo ni sehemu ya maandalizi ya awali kabla ya kuanza kwa shughuli rasmi za Bunge jipya baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Bunge la 13 linatarajiwa kujadili miswada kadhaa muhimu ikiwemo ile inayohusu mageuzi ya kiuchumi na utawala bora. Wataalamu wa siasa wanasema vikao vya mwanzo vitatoa mwelekeo wa namna Serikali itakavyotekeleza ajenda zake kuu za maendeleo katika kipindi kijacho cha miaka mitano.






0 Comments