Header Ads Widget

ESTHER MIDIMU ATEULIWA UBUNGE VITI MAALUMU.

 

Esther Midimu, Mbunge Mteule wa Viti Maalumu.


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imefanya uteuzi wa Wabunge Wanawaka wa Viti Maalumu 115 kati ya idadi ya Wabunge 116 wanaopaswa kuteuliwa, kufuatia masharti ya Ibara ya 66(1)(b) na 78 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, sambamba na kifungu cha 112 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024.


Tume hiyo ilifanya kikao chake leo Nov 7, 2025 ambapo ilikamilisha mchakato wa uteuzi wa Wabunge hao Maalumu ambao wanawakilisha makundi ya Wanawake kutoka vyama mbalimbali vya siasa vilivishiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.


Kutoka Mkoa wa Simiyu, walioteuliwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Tinar Chenge na Esther Midimu, huku Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikipata wabunge wateule wawili ambao ni Devotha Minja na Sigrada Mligo. 


Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI