Header Ads Widget

ACFE YAPONGEZWA KWA UDHIBITI WA VITENDO VYA UBADHILIFU.

 

Na,Jusline Marco:Arusha

Serikali imeipongeza Taasisi ya Wataalam wa Udhibiti wa Udanganyifu Tanzania (ACFE) kuwa ni nguzo muhimu katika kutambua, kuchunguza na kudhibiti vitendo vya ubadhilifu na udanganyifu katika sekta za Umma na binafsi nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya Maadili, Felister Shuli akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais , Utumishi wa Umma na Utawala bora wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Mwaka la ACFE Tanzania linalofanyika jijini Arusha na kusisitiza kuwa, ACFE imekuwa chachu katika kutoa mafunzo ya kimataifa na ushauri wa kitaalamu kwa wataalamu wanaohusika na kudhibiti udanganyifu.

Naye rais wa ACFE Tanzania, Ally Mabrouk Juma, amesema tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo, imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Wizara ya Fedha kupitia Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali katika kujenga uwezo wa wataalamu.

Ameongeza kuwa katika kongamano hilo, mada mbalimbali zinajadiliwa ikiwemo uchunguzi katika mazingira ya TEHAMA, mbinu za kisasa za kudhibiti udanganyifu katika teknolojia, uchunguzi wa utakatishaji fedha na uadilifu katika manunuzi na miradi ya maendeleo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI