Header Ads Widget

WANANCHI WA KATA YA BULYAKASHAJU WAWAANGUKIA WAGOMBEA UBOVU WA BARABARA YA NYAKAHAMA MPAKA RUHANGA

 

Na Mariam Kagenda _ Kagera 

 Wananchi wa kata ya Bulyakashaju wilayani Muleba wameomba viongozi watakaopata Ridhaaa baada ya kuchaguliwa na wananchi katika nafasi ya Ubunge  Jimbo la Muleba Kaskazini pamoja na diwani wa kata hiyo kuhakikisha wanatatua changamoto ya Barabara ya Nyakahama mpaka Ruhanga ili kupunguza adha wanayoipata kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Bulyakashaju Evodius Angelo,Edimundi Mishoshi  wakizungumza baada ya mkutano wa mgombea Ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini pamoja na mgombea udiwani kata ya Bulyakashaju kupitia Chama cha Mapinduzi wamesema kuwa barabara hiyo imekuwa changamoto ya muda mrefu hivyo viongozi watakaochaguliwa wanatakiwa kuanza kuboresha miundombinu ya barabara hiyo.

Wamesema kuwa wanatumia barabara hiyo kusafirisha mazao,kupeleka wagonjwa Zahanati lakini pia inatumika katika shughuli zao za kila siku hivyo kutokana na Ubovu uliopo upelekea kupitika kwa shida hasa wakati  mvua inaponyesha.

Kwa upande wake mgombea  udiwani  kata  ya Bulyakashaju Ponsian  Rwekaza amesema kuwa endapo wananchi wa kata hiyo watamchagua kuwa diwani wa kata hiyo atahakikisha anashirikiana na viongozi wengine pamoja na wananchi kutatua changamoto ya barabara hiyo kwani na yy ni mkazi wa kata hiyo hivyo anaifahamu vizuri kwani mvua zikianza kunyesha kuna maeneo hayapitiki kutokana na kujaa maji.

Naye  mgombea Ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini Bwana Adonis Bitegeko kupitia Chama cha Mapinduzi   amesema kuwa Ilani ya chama hicho imeeleza vyema namna itakavyotatua changamoto za wananchi ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara ambazo zina changamoto kwa wananchi wa Jimbo hilo .

Aidha amewaomba wananchi hao kukiamini Chama Cha Mapinduzi na kuwapigia kura viongozi wanaotokana na Chama hicho kwa Nafasi ya Mgombea Urais Dkt Samia Suruhu Hassan , Mbunge pamoja na madiwani ili waweze kutatua changamoto zinazowakabiri wananchi .



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI