Wakulima wa Morogoro wamevuna zaidi ya shilingi Bilioni 52 kutokana na mauzo ya mazao yao kupitia mfumo wa Stakabadhi za Ghalani na Soko la Bidhaa (TMX), hatua inayoliongeza kipato na kuleta mapinduzi ya kiuchumi mkoani humo.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, amesema mafanikio haya yamepatikana hasa katika mazao ya kakao, mbaazi, na ufuta.
Pia amesema matarajio ni kuwa zaidi ya shilingi Bilioni 200 zitaingia kwa wakulima wa Morogoro katika kipindi cha miaka minne ijayo, iwapo jitihada za kuimarisha mifumo ya masoko na usimamizi zitaendelea.
Aidha, Malima ameipongeza COPRA kwa kuhakikisha uwazi na usawa katika uuzaji wa mazao kupitia mifumo hii, hali iliyovutia wakulima wengi kuachana na njia za jadi na kujiunga na mfumo rasmi wa masoko.
0 Comments