Header Ads Widget

IRAN ILIONGEZA HIFADHI YA URANI HADI KIWANGO CHA SILAHA, SHIRIKA LA UN LINASEMA

 

Ripoti ya siri ya shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nyuklia ilisambazwa kwa nchi wanachama na kuonekana na Shirika la Habari la Associated Press ilisema Jumatano kwamba Iran iliongeza hifadhi yake ya madini ya urani yaliorutubishwa hadi kufikia viwango vya silaha kabla ya Israel kuanzisha mashambulizi yake ya kijeshi Juni 13.

Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) lenye makao yake makuu mjini Vienna imesema hadi kufikia Juni 13, Iran ilikuwa na kilo 440.9 (pauni 972) za uranium iliyorutubishwa hadi asilimia 60, ikiwa ni ongezeko la kilo 32.3 (pauni 71.2) tangu ripoti ya mwisho ya IAEA mwezi Mei.

Ripoti hiyo ilisema kwamba takwimu hii "inatokana na habari iliyotolewa na Iran, shughuli za uhakiki wa shirika hilo kati ya 17 Mei 2025 na 12 Juni 2025 (siku iliyotangulia kuanza kwa mashambulio ya kijeshi), na makadirio kulingana na operesheni ya zamani ya vituo husika."

Hatua hiyo imesalia kiwango kidogo tu kufikia silaha cha 90%.

Kulingana na IAEA, takriban kilo 42 za 60% ya madini ya urani iliyorutubishwa kinadharia inatosha kuzalisha bomu moja la atomiki, ikiwa itarutubishwa zaidi hadi 90%.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI