Ukraine imekataa pendekezo la Rais wa Urusi, Vladimir Putin, la kutaka Rais Volodymyr Zelensky asafiri kwenda Moscow kwa ajili ya mkutano wa pamoja kati yao.
Taarifa hiyo imeripotiwa leo na Shirika la Habari la Ujerumani, DW, likieleza kuwa Putin alitoa pendekezo hilo baada ya mazungumzo na Rais wa Marekani, Donald Trump, kufuatia mkutano wao wa kilele huko Alaska.
Akizungumza akiwa nchini China, Putin amesema Trump alimwomba kama kuna uwezekano wa kuandaa mkutano huo, na kwamba yuko tayari kumkaribisha Zelensky Moscow iwapo atakubali.
Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa X, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andrii Sybiha, amesema takribani nchi saba zimejitolea kuwa wenyeji wa mkutano huo na Zelensky yuko tayari kwenda katika mojawapo ya nchi hizo, lakini si Urusi.
0 Comments