Header Ads Widget

UKATILI WA KIJINSIA: BABA AMLAZIMISHA BINTI YAKE KUISHI NAYE KINYUMBA

Na Matukio Daima Media,Morogoro

TUKIO la kikatili la kijinsia limeibua mshangao na hasira kwa wakazi wa Kata ya Lukobe, Manispaa ya Morogoro, baada ya kubainika kuwa baba mwenye umri wa miaka 45, amekuwa akiishi kinyumba na binti yake wa kumzaa mwenye miaka 13, ambaye bado ni mwanafunzi wa darasa la saba.

Baba huyo, anayefahamika kwa jina la Stanley Kunambi, anadaiwa kumbaka na kumuingilia mtoto huyo kinyume na maumbile kwa muda mrefu, kitendo kilichoripotiwa polisi Septemba 1, mwaka huu.

Majirani waliokuwa wa kwanza kugundua hali hiyo wanasema waliona viashiria vya mahusiano yasiyo ya kawaida kati ya baba na binti yake.

“Tulianza kupata mashaka baada ya kuona mtoto anaishi chumba kimoja na baba. Hatukuamini hadi tulipoamua kutoa taarifa polisi,” alisema Evelyn Jonas, jirani wa familia hiyo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kambitano, Kata ya Lukobe, Eliamini Kimaro, amesema malalamiko hayo yaliwasilishwa rasmi na wananchi walioguswa na kitendo hicho cha kinyama.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea, huku jitihada zikifanyika kumtafuta mama mzazi wa mtoto ambaye alitengana na mtuhumiwa na kumwachia watoto wawili chini ya uangalizi wake.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI