Malawi inaelekea kwenye uchaguzi leo Jumanne utakaowakutanisha Rais Lazarus Chakwera na mtangulizi wake Peter Mutharika, huku nchi hiyo ikiendelea kukabiliwa na mfumuko wa bei uliokithiri na uhaba wa mafuta.
Wagombea wengine 15 akiwemo rais wa zamani Joyce Banda pia wanawania kiti cha urais, lakini wachambuzi wanatarajia kinyang'anyiro hicho kuwa kati ya wawili Chakwera, 70, na Mutharika, 85. Ikiwa hakuna atakayepata zaidi ya 50% ya kura, kutakuwa na duru ya pili.
Malawi imekabiliwa na mdororo wa kiuchumi tangu Chakwera kuchaguliwa mwaka 2020, huku kukiwa na kimbunga kikali na ukame uliofanya hali kuwa mbaya zaidi.
Kashfa za ufisadi zimechangia kukatishwa tamaa na pande zote mbili. Chakwera aliingia afisini akishutumu serikali ya zamani ya Mutharika kwa ufisadi uliokithiri, lakini usimamizi wake wa kesi umekosolewa kuwa wa kibaguzi na wa polepole.
Nchi yenye takriban watu milioni 22 pia itawapigia kura wabunge na madiwani wa mitaa leo siku ya Jumanne.
0 Comments