Header Ads Widget

TRILION 14 ZA RAIS SAMIA KIGOMA USIPIME


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKOA Kigoma unaelezwa kupokea kiasi cha shilingi Trilioni 14.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha miaka minne ya Raisi Samia Suluhu Hassan madarakani fedha ambazo zimeletwa mabadiliko makubwa ya maendeleo katika mkoa huo.

Naibu Waziri wa nchii ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Zainab Katimba amesema hayo katika uzinduzi wa kampeni ya mgombea ubunge wa jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma kwa tiketi ya CCM, Profesa Pius Yanda uliofanyika kwenye kijiji cha Muyama wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.


Naibu Waziri Katimba alisema kuwa fedha hizo zimekwenda kutekeleza ahadi aliyotoa Rais Samia ya kuufanya mkoa Kigoma kuwa mkoa wa Kimkakati kiuchumi na kwamba miradi mikubwa kwenye sekta ya miundo mbinu, biashara na uchumi ikiwemo masoko, elimu, kilimo, afya nay ale yote ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa kukuza uchumi wa mkoa Kigoma.

Akizungumza katika mkutano huo wa kampeni Mgombea ubunge wa jimbo la Buhigwe kwa tiketi ya CCM,Profesa Pius Yanda alisema kuwa moja ya mambo ambayo atayapa kipaumbele akiingia madarakani ni suala la kilimo akisimamia Zaidi kuimarisha zao la Tangawizi kulifanya zao kubwa la biashara.


Sambamba na hilo Profesa Yanda alisema kuwa suala la miundo mbinu pia litapewa kipaumbele hasa barabara kutoka maeneo ya kilimo yenye uzalishaji kwenda kwenye masoko ili kuwawezesha wananchi wa jimbo hilo ambao sehemu kubwa ni wakulima kuweza kusafirisha mazao yao kwa urahisi na kufanya kilimo chenye tija na kwamba masoko ya mazao pia yataimarisha

Akimnadi mgombea huyo Waziri wa zamani wa elimu, Profesa Joyce Ndalichako aliwaomba wananchi wa jimbo la Buhigwe kumchagua Profesa Yanda kwani ni mtaalam na bingwa wa kubuni miradi hivyo kuwa naye itakuwa rahisi kwake kubuni, kuitafutia fedha na kuisimamia miradi ya maendeleo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.


 


Mwisho.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI