Header Ads Widget

TOSCI YAWATAKA WAZALISHAJI MICHE NA MBEGU KUSAJILI VITALU NA MASHAMBA YAO

 


Na Lilian Kasenene,Morogoro 

TAASISI ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) imewataka wazalishaji wa Miche na mbegu kusajili mashamba na vitalu vyao.

Mkurugenzi wa TOSCI Nyasebwa Chimangu alisema lengo la kuwasajili wazalishaji hao ni kuwasaidia wakulima kupata mbegu na Miche Bora.

"Baada ya serikali kutafuta masoko ya parachichi kwenye nchi mbalimbali hivi Sasa Tanzania imekuwa nchi ya tatu kwa uzakishaji wa zao hilo hivyo ni muhimu kuwa na mbegu bora," alisema. 


Chimangu aliwaeleza waandishi wa habari kuwa hadi Sasa TOSCI imesajiri aina tano za mbegu za parachichi zenye ubora na viwango vinavyohitajika


"Wakulima watumie mbegu za parachichi watumie mbegu halisi zenye ubora ili kupata matunda yatakayohimili ushindani kwenye soko la kimataifa,"alisema mkurugenzi Chimangu.



Alisema kwa Sasa Parachichi za Tanzania zinauzwa kwenye nchi za China, Afrika Kusini, India, Uingereza na nchi za Karibia na kote huko wanazingatia ubora wa kuanzia kwenye mbegu na Miche.


Chimangu alisema ili kupata matokeo sahihi ni lazima wazalishaji wa mbegu na Miche wasajili bitalu na mashamba yao Ili wapatiwe mafunzo kutoka TOSCI.


Pia mkurugenzi huyo aliwataka wakulima wanapohitaji kununua mbegu au Miche wahakikishe Zina nembo ya TOSCI ili kujiridhisha na ubora wake.


Alisema ivi Sasa wanafanya ukaguzi kwenye mashamba na vitalu watakaobainika kuuza Miche na mbegu zisizo na nembo ya TOSCI watachukuliwa hatua za kisheria.


Mmoja wa wanufaika wa mafunzo ya uandaaji wa mbegu na Miche kutoka TOSCI Tolli Lishera alisema baada ya kusajiliwa wateja wake wameongezeka kutoka na kuwa na Miche na mbegu za kuaminika


"Wakati nazalisha kienyeji ukiwauzia Miche wateja wasipopata matokeo sahihi hawarudi kununua ila sasa wateja wenyewe ndio wananitangazia masoko,"alisema Lishera.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI