Header Ads Widget

PROF. KIHAMPA ATANGAZA IDADI YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU

 

Na mwandishi wetu

Awamu ya kwanza ya udahili wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026 imefungwa rasmi leo, ambapo waombaji zaidi ya laki moja na kumi na sita wamethibitishwa kujiunga na vyuo vikuu nchini.

Akizungumza Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Charles Kihampa amesema jumla ya waombaji 116,596 wamedahiliwa katika taasisi 88 za elimu ya juu nchini.

Kati yao, zaidi ya 67,000 wamechaguliwa katika chuo au programu zaidi ya moja, na hivyo wanatakiwa kujithibitisha katika programu na chuo kimoja kuanzia leo Septemba 3 hadi 21, ili kutoa nafasi kwa waombaji wengine.

Profesa Kihampa amesema hatua hiyo itatoa nafasi kwa wanafunzi ambao hawakupata nafasi katika awamu ya kwanza kuomba tena kwenye awamu ya pili ya udahili, ambayo inaanza leo na kuhitimishwa Septemba 21.

Aidha, amebainisha kuwa kwa mwaka huu taasisi za elimu ya juu zina jumla ya nafasi 205,652, ikiwa ni ongezeko la nafasi 6,666 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI