Na mwandishi wetu
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Mwalimu Mkuu na mlinzi wa Shule ya Msingi Ngarenaro kwa tuhuma za kumfanyia ukatili mwanafunzi wa darasa la saba, wakidai kuwa mtoro.
Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, amesema watuhumiwa hao ni Mwalimu Mkuu Mussa Luambano (50) na mlinzi Olais Mollel (33), ambao wanadaiwa kumfunga kwa mnyororo na kufuli mwanafunzi Hussein Juma (13) kwenye dawati na kumfungia darasani, Septemba Mosi.
Tukio hilo limeelezwa kutokea baada ya mwanafunzi huyo kudaiwa kuwa mtoro, ambapo mama yake, Amina Juma, amesema mtoto wake aliitwa shuleni kwa maandalizi ya mitihani licha ya kuwa anaumwa.
Kamanda Masejo amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea, na baada ya kukamilika, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watuhumiwa.
0 Comments