Header Ads Widget

MWENDESHA MASHTAKA AOMBA KABUGA AREJESHWE RWANDA

 

Mwendesha mashitaka wa kitengo cha Mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR) kilichosalia kusikiliza kesi zilizoachwa na Mahakama hiyo ya Arusha amekitaka kitengo hicho kufanya utafiti wa kuachiwa kwa muda kwa Félicien Kabuga na kuhamishiwa Rwanda, nchi alikozaliwa ambayo "ndio pekee imeonyesha nia ya kumpokea", kwa mujibu wa waraka kutoka katika kitengo hicho.


Kwa sasa Kabuga anazuiliwa katika gereza la The Hague, Uholanzi, baada ya chumba cha taasisi inayofanya kazi huko mnamo mwezi Septemba, 2024 kuamua kusitisha kwa muda usiojulikana kesi ya Kabuga mwenye umri wa miaka 90 kwa misingi ya afya, na kwamba ataachiliwa kwa dhamana.


Kabuga alishtakiwa kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa kifedha kwa mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda, mashtaka aliyoyaita "uongo".


Jumanne mjini Arusha, Tanzania, jopo la majaji watatu; Iain Bonomy, Mustapha El Baaj na Margaret M. deGuzman na ripota Bw. Abubacarr M. Tambadou msajiliwa mahakama walijadili kuhusu kuachiliwa kwa muda kwa Kabuga na kurejeshwa Rwanda.


Hati hiyo ya mahakama inasema kwamba kutokana na matukio ya miaka miwili iliyopita, “Kabuga akiachiliwa atakwenda Rwanda pekee”.


Redio ya Ufaransa RFI inaripoti kwamba wakili wa Kabuga alijaribu kuuliza moja ya nchi za Ulaya kumkubali. Lakini , hata Ufaransa, nchi ambayo alikamatwa mwezi Mei, 2020 baada ya miaka 26 ya kuwa mafichoni haijakubali kumkaribisha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI