Mkurugenzi wa Taasisi inayowezesha mifumo ya ajira Nchini Dproz .com.Iddy Magohe amesema iko changamoto ya ajira hususani vijana wanaotafuta ajira lakini sababu kubwa ni ukosefu wa taarifa ya ajira ambazo zinapatikana
Amesema watu wengi wanaomba nafasi za kazi ambazo zinajulikana sana huku akitolea mfano Mamlaka ya mapato TRA hivi karibuni ili tangaza nafasi za ajira kama 1800 mpaka 1900 lakini waliokuwa wamepeleka Maombi ni zaidi watu laki Moja ambapo hao wote bado wako kwenye soko la Ajira
Magohe ameyabainisha hayo hivi karibuni jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari juu ya umuhimu wa kutumia mfumo wa Dproz kuweza kupata taarifa za kipaji Cha soko la ajira .
Amesema kama Dproz wana Kampuni zingine mbalimbali ambazo wanazisaidia kupata watu na wametangaza kazi lakini hazipati Maombi hivyo manaake Kuna watu wako kwenye soko la ajira lakini hawapati taarifa .
Magohe amefafanua kuwa mfano watu wameomba kazi na hakufanikiwa kupata lakini kama angekuwa yuko kwenye mfumo wa diproz angeweza kupata taarifa nyingine za soko la ajira hivyo wao kazi yao ni moja tu kujilisha Vipaji uwepo wa soko la ajira .
Amesema lengo kubwa la Dproz nikuona nafasi yeyote ambayo Iko wazi inamfikia mtanzania na anapofuatilia soko la ajira kupitia Dprozi haitaji kutembeza bahasha au kumaliza soli za viatu kwenda kutafuta kazi.
Ameongeza ni vema mtanzania kama unakipati na unafikiri kuingia kwenye soko la ajira basi tafuta taarifa kupitia Dproz na ukishajiunga tu yenyewe inaaza kukupa taarifa ya soko la Kazi
Amesema pia hata kama upo chuoni unaweza kujiunga huku akiitaka Serikali kuendelea kushirikiana na Sekta binafsi ili kuweza kusaidia kujua kipaji Cha mtu pindi anaingia kwenye soko la ajira .
Akizungumzia vijana ambao wanatoka vyuoni au wako vyuoni kujua njia gani ambayo wanaweza kupitia ili kujua soko la ajira likoje na ni utalaamu upi ambao uko sokoni jibu lake dproz.
Magohe ameongeza kuwa Dproz pamoja na mambo mengine lakini wao kama taasisi wanahakikisha wanamshika mkono kijanà au mtu hadi pale kwa namna moja ama nyingine atakapoonekana amefanikiwa .
Akizungumzia wanavyoshirikiana na Serikali amesema bado hawajangia moja kwa moja lakini wanaamini huko mbele wataweza kushirikiana ipasavyo ili kuongeza ufanisi na hasa hatua ya kuchagua ni akina nani wanaweza kuingia kwenye usahili .
Amesema ajira zipo ila watu wahakikishe wanapata taarifa na sehemu ya kupata taarifa ni kufuatilia na kuingia kwenye mifumo ya Dproz ,ambapo inafikika kupitia www.dproz.com au kwenye Dproz App katika Google Play Store.
0 Comments