Header Ads Widget

KIONGOZI MBIO ZA ATOA USHUHUDA ALIYOFANYA RAIS SAMIA

 

Mkuu wa wilaya Kakonko Evance Malasa (kulia) akikabidhi mwenge wa uhuru kwa mkuu wa wilaya Kibondo Agrey Mwagaza (kushoto) ili mwenge huo uanze mbio zake wilayani Kibondo jana baada ya kumaliza ratiba yake katika wilaya ya Kakonko.

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru Ismail Alli Ussi amesema kuwa miradi mbalimbali  inayotekelezwa na serikali imeleta mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo kwa wananchi ikitekeleza falsa na maono ya Raisi katika kuleta hali bora ya maisha kwa wananchi.

Ussi alisema  hayo wilaya Kibondo mkoani Kigoma katika siku ya pili ya ziara ya siku nane ya mwenge wa uhuru mkoani Kigoma  ambapo alisema kuwa anashangazwa na watu wanaobeza kuwa serikali haijafanya kitu.

Wakimbiza Mwenge wa uhuru Kitaifa wakiongozwa na Kiongozi wa Mwenge wa uhuru mwaka huu Ismail Alli Ussi wakishuhudia ukaguzi wa ubora wa barabara kwa kutumia mashine ya ubora  kunakofanywa na watendaji wa barabara za mjini na vijijini (TARURA) wakati wa ukaguzi wa barabara ya kiwango cha lami ya uswahili mjini Kibondo yenye urefu wa mita 470.

Kiongozi huyo  ambapo alibainisha kuwa Rais Samia anamapenzi makubwa na wananchi wake ndiyo maana anapambana kuhakikisha wanapata maendeleo.

Ukiwa  wilayani Kibondo mwenge wa uhuru ulizindua madarasa manne na matundu sita ya vyoo katika shule mpya ya msingi Kilemba, uwekaji wa jiwe la msingi la barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa mita 470, kuweka jiwe la msingi la vibanda 66 vya biashara kwenye soko la samaki Kibondo mjini sambamba na ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Maloregwa.


Mkuu wa wilaya Kibondo Agrey Magwaza (kulia) akimuongoza Kiongozj wa Kitaifa wa Mwenge wa uhuru mwaka 2025 Ismail Alli Usi (kushoto) kukagua madarasa ya Shule mpya ya Msingi ya  Kilemba wilayani Kibondo wakati mwenge wa uhuru ulipokuwa ukizindua madarasa hayo.

Awali Mkuu wa wilaya ya Kibondo,Kanali Mstaafu Agrey Magwaza  akipokea kwenye wa uhuru kutoka wilaya ya Kakonko alisema kuwa ukiwa wilayani humo mwenge huo wa uhuru utatembelea miradi saba yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.1 ambapo serikali kuu imetoa kiasi cha shilingi bilioni 2.1 na nguvu za wananchi shilingi milioni 16.

Akiwa kwenye mradi wa ujenzi wa vibanda kwenye soko la samaki Kibondo Mjini Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa katika mradi huo jumla ya vibanda 66 vinajengwa sambamba na meza ambapo wafanyabiashara Zaidi ya 200 wanatarajia kunufaika na uboreshaji wa soko hilo.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI