Header Ads Widget

ESTER MIDIMU AKOLEZA MOTO AKIMNADI NJALU SILANGA.

ESTER Midimu ambaye ni Mbunge Mteule wa Viti Maalumu kupitia CCM, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga.
 

Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.


ESTER Midimu ambaye ni Mbunge Mteule wa Viti Maalumu kupitia CCM, amewataka wananchi wa Jimbo la Itilima kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Njalu Silanga pamoja na Mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Hassan ili waendelee kuwatumikia. 


Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni uliofanyika Kijiji cha Nangale, Midimu amesema kuwa katika miaka mitano iliyopita, Njalu ameboresha huduma za kijamii ikiwemo kusimamia ujenzi wa zahanati, vituo vya Afya na Hospitali. 


"Njalu ameiomba fedha kwa Rais Dk. Samia zaidi ya shilingi Bil. 4 tukajenga Hospitali ya wilaya ambayo inatumika, pia akaomba fedha Shilingi Bil. 3.6 ya dawa na vifaa tiba.. tumpeni kura za kishindo Njalu pamoja na Rais Dk. Samia ili wachape kazi na kutuletea Maendeleo" amesema Midimu. 


Mwisho.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI