Header Ads Widget

BARABARA ZA VIJIJINI KAGERA ZAIMARIKA :TARURA YAKARABATI KILOMITA 1409 KWA BILIONI 24.7

 

Na Shemsa Mussa -Matukio Daima Media 

                    Kagera.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Kagera umetumia jumla ya shilingi bilioni 24.7 katika mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya matengenezo ya barabara na karavati katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

Kwa mujibu wa Meneja wa TARURA Mkoa wa Kagera, Mhandisi Wilson Mwita, amesema Mkoa ulikuwa na mpango wa kutengeneza barabara zenye urefu wa kilomita 6402, ambazo zimesajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii.

Hadi sasa, TARURA Kagera imefanikiwa kutengeneza kilomita 1409 kati ya zilizopangwa, hatua inayowakilisha mafanikio ya asilimia 80 ya utekelezaji wa lengo la mwaka huu wa fedha.


Mhandisi Mwita amesema kuwa kati ya kilomita zilizotengenezwa, kilomita 1130 zipo kwenye viwango mbalimbali vya ujenzi, ikiwa ni pamoja na barabara za rami, changarawe na udongo

Amefafanua kuwa kilomita 9.2 zimetengenezwa kwa kiwango cha lami (rami), kilomita 585 kwa kiwango cha changarawe, huku kilomita 816 zikiwa ni za kiwango cha udongo.

Mbali na barabara, TARURA pia imetengeneza makaravati 685 katika maeneo mbalimbali ya mkoa, ikiwa ni sehemu ya kuboresha miundombinu na kuongeza upitikanaji wa watu na bidhaa.

Meneja huyo amesema kazi hizo zinalenga kupunguza changamoto ya usafiri hasa katika maeneo ya vijijini, na kuboresha huduma za kijamii kama vile afya, elimu na uchumi na huduma nyinginezo.

Ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na TARURA katika kulinda miundombinu hiyo kwa kutoruhusu shughuli zinazoharibu barabara, kama kuchimba mifereji kiholela au kuweka taka kwenye mifereji ya maji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI