Header Ads Widget

WAJASIRIAMALI WADOGO WAASWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII


Na Samwel Mpogole 

Wajasiriamali wadogo wadogo nchini wamekumbushwa umuhimu wa kujiandaa mapema kwa kuwekeza akiba katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili kujihakikishia maisha bora wanapofika uzeeni au kukumbwa na changamoto za kiafya na majanga.

Akizungumza jijini Mbeya, Afisa Mwandamizi Mkuu wa Mafao na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Yohana Mwambilija, alisema NSSF imeanzisha Mfuko Maalum wa Hifadhi Skimu unaolenga kuwasaidia watu wenye kipato cha chini kujiwekea akiba kwa gharama nafuu.

Alifafanua kuwa mpango huo unawawezesha wanachama kujiandaa na maisha ya baada ya kustaafu, kuepuka changamoto za kifedha, na kuhakikisha wanaendelea kuishi kwa heshima hata wanapopoteza uwezo wa kufanya kazi.

Kwa upande wake, Ibrahim Nganga, Afisa Mwandamizi wa NSSF mkoani Mbeya, alisema mfuko huo wa akiba unatoa faida nyingi zikiwemo msaada wa kifedha wakati wa uzee, msaada wa matibabu, na fidia katika tukio la majanga.

“Nia yetu ni kuhakikisha kila mwananchi, hususan wajasiriamali wadogo, anakuwa na usalama wa kifedha kwa maisha ya baadaye,” alisema Nganga.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI