Na Leonard Johnson
Baada ya mchezo wa timu ya Taifa la Kenya [ Harambee stars] dhidi ya Timu ya taifa la Angola kumalizika kwa matokeo ya sale ya 1-1 katika mchezo wakundi " A " hapo jana ,wachezaji wamepata ofa nono kutoka kwa Rais wao William Ruto kiasi cha fedha thamani ya laki tano ambayo ni sawa na mil 10 ya kitanzania ,awali wachezaji waliwekewa fedha sh.mil 1 ambayo ni sawa na mil 20 za kitanzania endapo wangeshinda mechi hiyo.
Hata hivyo,timu ya Harambee Stars pamoja na matokeo hayo inaendelea kushika nafasi ya kwanza katika kundi " A" ,wakiwa na alama 4,michezo 2 ,wakifuataiwa na Morocco alama 3,mchezo 1 nafasi ya tatu ikishikiliwa na Congo alama 3,michezo 2 ,nafasi ya 4 Angola alama 1,michezo 2 na Zambia ikibuluza mkia kwa alama 0,mchezo 1.
Katika mchezo huo kulizua hisia nzito kwa wapenzi wa soka barani Afrika kwa tukio la harambee stars kupata kadi nyekundu dakika za mwanzoni mwa mchezo huku wakiwa wamesha fungana 1-1 ,nakucheza pungufu ya watu kumi huku Angola wakiwa wameenea lakini Harambee stars walionyesha ushindani mkubwa wenye hadhi ya mashindano.
0 Comments