Na Matukio Daima Media, Morogoro
Vibaka waliokuwa na silaha zenye ncha kali wamevamia na kuwajeruhi watu watatu akiwemo mfanyabiashara wa huduma za kifedha, Benjamin Erasto, katika Mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kihonda katika Manispaa ya Morogoro.
Benjamin Erasto ni mfanyabiashara wa huduma za kifedha anayefanya shughuli zake katika eneo la NK Mazimbu road, kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo wahalifu hao walipora fedha zaidi ya shilingi milioni mbili na laki Tano, simu na mashine za kutolea huduma.
Mashuhuda wamesema tukio hilo lilifanyika kwa kasi na ujasiri mkubwa, huku waathirika wa tukio hilo wakinusurika kifo.
Polisi wameanza uchunguzi lakini bado hakuna mtu aliyekamatwa.
0 Comments