Ni karibu 08:30 huko Jerusalem na 06:30 London. Usiku kucha, tumekuwa tukifuatilia matukio nchini Israel, ambapo baraza la mawaziri la usalama la nchi hiyo limeidhinisha mpango wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa kulikalia jiji la Gaza.
Ikiwa unajiunga nasi sasa hivi, haya ndiyo unayohitaji kujua:
Baraza la mawaziri la usalama la Israel liliidhinisha kutwaliwa kwa mji wa Gaza kwa kura nyingi Inaashiria kuongezeka kwa vita vya karibu miaka miwili na inaweza kuwa awamu ya kwanza ya utekaji kamili wa Gaza na jeshi, mwandishi wetu wa Mashariki ya Kati Hugo Bachega anasema.
Hapo awali Netanyahu alisema anataka kuchukua eneo lote la Ukanda wa Gaza lakini mpango ulioidhinishwa unalenga hasa mji wa Gaza, mji mkubwa zaidi katika eneo hilo.
Mpango huo umeibua maonyo kutoka kwa uongozi wa jeshi, upinzani kutoka kwa familia za mateka na wasiwasi kwamba Wapalestina zaidi watauawa.
Pia kuna hatari ya kuitenga Israeli hata zaidi kimataifa.
Umoja wa Mataifa umeonya hapo awali kwamba Israel kupanua operesheni za kijeshi kunahatarisha "matokeo mabaya" kwa raia wa Palestina na mateka wa Israeli.
0 Comments