Header Ads Widget

UJENZI RELI YA KISASA SGR UVINZA HADI MSONGATI WAANZA RASMI

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa (wa tatu kulia) na Raisi wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayishimiye (kushoto) wakisalimiana wakati wa hafla ya  kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Msongati mkoa Burunga nchini Burundi kuelekea Uvinza mkoani Kigoma nchini Tanzania.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa (wa pili kushoto) na Raisi wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayishimiye (wa pili kulia) wakichanganya udongo na kufungua pazia ikiwa ishara ya kuweka rasmi jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Msongati mkoa Burunga nchini Burundi kuelekea Uvinza mkoani Kigoma nchini Tanzania

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la reli nchini Machibya Masanja (katikati) akitoa maelezo kwa Raisi wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayishimiye (wa pili kulia) na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa (kushoto) kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa SGR kutoka Uvinza mkoani Kigoma nchini Tanzania hadi Msongati mkoa wa Burungu nchini Burundi


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Tanzania na Burundi zimeweka historia mpya katika diplomasia ya uchumi na uhusiano baada ya kuwekwa kwa jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya Kisasa kutoka Uvinza mkoani Kigoma hadi Msongati nchini Burundi.

 

Uwekaji wa jiwe la Msingi umefanyika katika eneo la Msongati mkoa wa Burungu nchini Burundi ambapo uwekaji huo wa jiwe la Msingi uliongozwa na Raisi wa Burundi, Evariste Ndayishimiye na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwakilisha Raisi Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.

 

Akizungumza katika uwekaji huo wa jiwe la Msingi mkoa Burungu nchini Burundi Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo ni hatua kubwa kwa nchi hizo katika kuimarisha diplomasiaa ya uchumi lakini pia mahusiano ya kindugu yaliyopo baina ya nchi hizo mbili.

 

Majaliwa alisema kuwa mradi huo utachochea ukuaji wa uchumi kwa nchi hizo mbili, kuchochea ukuaji wa uchumi wa kikanda kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo utakuwa kichocheo kikubwa katika ukuaji wa sekta ya biashara, kilimo, viwanda na  madini.

 


 

Akizungumza katika Hafla hiyo Raisi wa serikali ya Burundi, Evariste Ndayishimiye alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo ni jambo kubwa kiuchumi kwa nchi hiyo katika kusafirisha mizigo hasa madini ya Nikel ambayo yanapatikana kwa wingi katika eneo hilo la Msongati mkoa Burungu nchini  Burundi lakini hayakuwa yakichangia sana uchumi wa nchi hiyo kwa kukosa miundo mbinu ya kuyasafirishia.

 

Alisema kuwa serikali ya Tanzania imekuwa na undugu na urafiki wa damuna Burundi ambao uhusiano huo umetoka kuwa urafiki wa kindugu na kuhamia kwenye masuaala ya uchumi na biashara mambo ambayo yanaleta manufaa kwa wananchi wa nchi hizo mbili.

 

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la reli nchini (TRC), Machibya Masanja alisema kuwa uwekaji wa jiwe hilo la msingi unahusisha utekelezaji wa mradi wa reli ya kisasa yenye urefu wa kilometa 190 kutoka Uvinza mkoani Kigoma nchini Tanzania hadi Msongati mkoa wa Burungu nchini Burundi wenye thamani ya Dola Zaidi ya Milioni mbili za Marekani ukiwa mradi wa miaka sita.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI