MWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali George Marwa Waitara amepokea tuzo ya kutambua mchango wake katika kuendeleza na kusimamia shughuli za uhifadhi katika Hifadhi za Taifa nchini.
Tuzo hiyo amekabidhiwa leo Agosti 14, 2025 na Mjumbe wa Bodi ya TANAPA Dkt. Robert Fyumagwa ambaye aliipokea kwa niaba yake katika maadhimisho ya siku ya Askari Wanyamapori Duniani (World Ranger’s Day) iliyoadhimishwa mnamo Julai 31, 2025 katika Hifadhi ya Taifa Tarangire.
0 Comments