Header Ads Widget

RAIS DKT SAMIA AZINDUA KITUO CHA EACLC, ATOA WITO KWA WAZALISHAJI WA BIDHAA ZA NDANI

 

Na Mtumwa Ali, 

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka wazalishaji wa bidhaa za ndani nchini humo kuzalisha bidhaa zenye viwango vinavyokubalika.

Wito huo ameutoa leo jijini Dar es salaam wakati akizindua mradi wa uwekezaji wa kituo Cha biashara na usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) ambapo mradi huo ulianza kutekelezwa mnamo Mei 2023, ambapo umegharimu shill bill 282.7 hadi kufikia hatua ya kukamilika.

Amesema kuwa, bidhaa yoyote itakayozalishwa nchini Tanzania au itakayotoka na nembo au alama ya nchi hiyo ni lazima iwe na viwango vilivyokubalika kama lilivo jina la Tanzania .

Aidha amesema uzinduzi wa kituo hicho umefanyika baada ya Jana Julai 31, kufanyika kwa uzinduzi wa kituo cha Logistics cha kwala na kuzinduliwa kwa safari za mizigo kwa kutumia reli ya MGR.

"Mradi huu ni wa kimkakati katika kutatua changamoto nyingi za biashara zilizokuwa zikiikabili nchi ya Tanzania na nchi jirani kwa muda mrefu"

"Masuala ya miundombinu rafiki,ucheleweshaji  wa mizigo na gharama kubwa za uendeshaji za biashara zinakwenda kutafutiwa ufumbuzi kwa miradi iliyozinduliwa Jana na Leo"

Ameongeza kupitia kituo hicho wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi wataweza kufanikisha shughuli zao kwa urahisi zaidi kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kidigital.

"Kwa Msingi huo ninawapongeza sana wawekezaji kwa ujenzi wa kituo cha kisasa cha biashara na usafirishaji ambacho kitakuza biashara na uwekezaji kati ya sekta binafsi za Tanzania na China.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuwa katika kusimamia mradi huo wamejipanga kuhakikisha umeme upo wa kutosha ili kuhakikisha shughuli zote zinafanyika bila tatizo lolote.

Aidha, Chalamila amewatoa wasiwasi wawekezaji na wafanyabiashara na usafirishaji Afrika Mashariki EACLC kuwa umeme hakutokua tatizo katika kituo hicho.

Amesema Dar es Salaam ina miradi zaidi ya minne ya kuzalisha umeme jambo ambalo litamaliza tatizo ndani ya mkoa na kurahisisha shughuli katika kituo hicho Cha biashara na usafirishaji Afrika Mashariki.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na maeneo Maalum ya kiuchumi (TISEZA ) Gilead Teri amesema kuzinduliwa kwa kituo hicho ni kufungua historia mpya kati ya China na Tanzania pamoja na kuwavutia wawekezaji ndani na nje ya nchi.

Kituo Cha mradi wa uwekezaji wa kituo cha biashara na usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) mpaka sasa kina wafanyabiashara 400 ambao wameshachukua maduka huku wanaohitajika ni 2060.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI