Header Ads Widget

MVELLA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI KATA YA MKIMBIZI AAHIDI KUENDELEZA MAENDELEO.

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

IRINGA.Mgombea Udiwani kata ya Mkimbizi Eliud Mvella kupitia chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Iringa Leo amefika katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi katika kata hiyo kuchukua fomu kwa ajili ya kupeperusha bendera ya chama hicho baada ya kuteuliwa na kamati kuu.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu Mvella amesema kuwa anawashukuru wagembea wenzake waliochukua fomu na mpaka sasa chama kimeteua mtu mmoja wa kuweza kupeperusha bendera ya CCM ili aweze kuleta maendeleo katika kata hiyo.

Mvella alisema kuwa yeye ambaye leo  ameteuliwa sio kwamba ni bora kuliko wengine ambao hawajateuliwa, bali wote walikuwa na nia na malengo lakini mfumo wa uongozi hamuwezi kuongoza watu wote.

Mvella alisema kuwa lengo la kugombea ni kuhakikisha anaendelea kuleta maendeleo katika kata ya Mkimbizi kwa kushirikiana na serikali pamoja na wananchi na wadau mbalimbali  

Alisema kuwa katika siasa na uongozi kila mtu anayohaki ya kumpenda na kumchagua kiongozi anayeona anafaa, hata katiba imeruhusu kwamba unapochagua unajua huyu atanisaidia, kupenda kumpigia kampeni mtu mwingine sio kosa.

"Inapofika chama kimeteua mtu mmoja wa kugombea tuungane wote pamoja, mimi nasema wale ambao niliwakosea wanisamehe, na wale walionikosea mimi nimewasamehe kwa kuwa natambua uchaguzi ni mchakato, nawaomba wanachama na wananchi tuungane pamoja na kuvunja makundi tupaoelekea uchaguzi mkuu 2025"

Mvella alisema kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi hivyo wasahau yaliyopita na kuendelea kukijenga chama kwa maslahi ya kuleta maendeo katika kata ya Mkimbizi.

"Awamu iliyopita ya udiwani kulikuwa na shida ya miundombinu, afya, umeme, maji na mambo mbalimbali  ambayo yamekamilika kwa asilimia 80 katika kata ya Mkimbizi"

Alisema kuwa kwa awamu hii ndani ya miaka mitano atahakikisha ameongeza shule ya sekondari, barabara ndogo ndogo za ndani ya kata,na ninatarajia kufanya ujenzi wa lami kuanzia Mkimbizi hadi Mtwivila na mikakati imekamilika na ujenzi utaanza mwezi ujao.

"serikali imeweza kutusaidia fedha zaidi ya Bilion 12 kwa ajili ya ujnzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami, barabara kubwa tayari zimekamilika zilizobaki ni barabara ndogo ndogo ambazo naamini kwa kushirikiana na TARURA tutatengeneza mpango na kuhakikisha barabara zinatengenezwa, huku ilani Mpya inakuja na imeweka mkazo katika ukarabati na ujenzi wa shule za msingi na sekondari"alisema 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Mkimbizi Omary Mwivila alisema kuwa hawana diwani mwingine isipokuwa Eliudi Mvella na wao kama wawakilishi wa kamati ya siasa na kamati ya kampeni mtu watakaye mnadi kwasasa ni Eliudi Mvella.

"Wanachama na wananchi wa kata ya Mkimbizi tunaushirikiano ndio maana kata yetu inamendeleo na tunatarajia maendeo zaidi baada ya ushindi oktoba 29,2025"alisema

Naye kwa niaba ya Kinamama wa kata ya Mkimbizi wanayofuraha kumsindikiza diwani kuchukua fomu kwani lengo lake kubwa ni kuleta maendeleo katika kata ya Mkimbizi.

"Tunafuraha kuona diwani wetu ameteuliwa tena kugombea nafasi hii kwetu ni furaha kwa kuwa tumeona aliyoyafanya katika kipindi cha miaka mitano na tunaendelea kujifunza na kata zingine ziige mfano kwa kazi anazozifanya" alisema 

MWISHO.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI