Header Ads Widget

MAVUNDE - UZALISHAJI VIWANDA VYA NDANI MUHIMU KWA UCHUMI WA NCHI

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WAZIRI wa madini Anthony Mavunde amesema  kuwa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali unaofanywa na wawekezaji wa ndani kwa ajiili ya matumizi ya ndani yana faida kubwa katika kupunguza matumizi ya fedha za kigeni katika kuagiza midhaa kutoka nje ya nchii.

Waziri Mavunde alisema hayo akizindua bidhaa mpya ya Chumvi Lishe kwa ajiili ya mifugo inayozalishwa na kiwanda cha Nyanza Salt Mines cha Uvinza mkoani Kigoma ambapo alisema kuwa bidhaa hiyo ni ya kwanza kuzalishwa nchini.


Alisema kuwa kabla ya kuzinduliwa kwa bidhaa hiyo Tanzania ilikuwa ikiagiza nje ya nchi chumvi lishe ambayo haikuwa ikizalishwa popote nchini na kwamba uzalishaji huo utatibu changamoto kubwa ya upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa wafugaji nchini na kuwataka wafugaji kutumia chumvi hiyo ya uvinza badala ya kuagiza nje.

Sambamba na hilo Waziri Mavunde amekipongeza kiwanda cha Nyanza Salt Mine kwa upanuzi wa kiwanda hicho katika uzalishaji wa chumvi kwa ajili ya matumizi ya binadamu ambapo uzalishaji huo utapanda kufikia tani 120 miaka miwili ijayo kutoka tani 80 zinazozalishwa sasa jambo litakaloifanya nchi kujitosheleza kwa chumvi.


Akizungumza mbele ya Waziri wa madini Mkurugenzi Mtendaji wa Nyanza Salt Mines, Mukeshi Mamlani alisema kuwa kiwanda hicho  ni mzalishaji wa kwanza wa Chumvi Lishe inaayotumika kwa mifugo na kwamba hiyo inatokana na fursa waliyoina katika soko ambako bidhaa hiyo imekuwa ikiagizwa kutoka nje hivyo kuwepo kwa mahitaji kwa wafugaji na soko kwa upande wao.

Mukeshi alisema kuwa mpango wa kiwanda hicho ni kuzalisha chumvi lishe ya kutosha kwa ajili ya mahitaji ya nchi nzima na kwamba Kampuni hiyo inatarajia kuwekeza kiasi cha Shilingi  bilioni 20 kwa ajili ya uzalishaji wa chumvi hiyo na upanuzi wa kiwanda hicho.

Pamoja na hilo Mkurugenzi huyo amemuomba Waziri huyo wa madini kuangalia namna ya kupunguza kodi na masharti mbalimbali kwa ajili ya  uzalishaji na uchakataji wa chumvi ili masharti hayo yasilingane na madini mengine yanayochimbwa nchini lakini pia iweze kusaidia kukusa sekta ya chumvi inayozalishwa ndani ya nchi.


Akitoa salamu mbele ya Waziri wa madini, Mkuu wa wilaya Uvinza mkoani Kigoma, Dinnah Mathaaman alisema kuwa kuwepo kwa kiwanda hicho mkoani humo kimekuwa na msaada mkubwa kwani imetoa ajira kwa wananchi 150 lakini pia imekuwa ikitoa ajira za muda za mikataba Zaidi ya 1000 wakati wa uvunaji chumvi sambamba na kuiingizia serikali mapato kwa kodi na ushuru mbalimbali.






 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI