Header Ads Widget

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WAZALISHAJI WA MAUDHUI MTANDAONI WANOLEWA NA TUME HURU YA UCHAGUZI

  

Na Fatma Ally Matukio Daima Media

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufani), Jacobs Mwambegele amewataka wazalishaji maudhui mtandaoni kutokua chanzo cha kusambaza taarifa za kuleta taharuki hasa kuelekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu Octoba 2025.



Hayo ameyaeleza leo jijini Dar es Salaam wakati walipokutana na wazalishaji wa maudhui mtandaoni ambapo amesema wapo watu walenye nia ovu hutumia akili under kusambaza habari za upotoshaji kupitia mitandao haswa ya kijamii.


Aidha, amewataka wazalishaji wa maudhui mtandaoni kuepuka matumizi ya mabaya ya akili unde kusambaza taarifa za upotoshaji kupitia mitandao ya kijamii kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.

 

"Natoa wito kwenu kuhakikisha taarifa mnazizoweka katika kurasa zenu ni za kweli na sisizo na chembe ya upotoshaji kwa kuwa ukosefuwa umakini kwenye eneo hili unaweza kuharibu na kuvuruga kabisa amani na utulivu wa nchi yetu wakati huu wa Uchaguzi,"amesema.

Amefafanunua kuwa, Tume ina matumaini makubwa ya kufanikisha Uchaguzi huo kwa kutegemea ushiriki wao kutokana na ushiriki wao wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.



"Mmekuwa wepesi wa kuwasilisha hoja na ushauri na kutaka ufafanuzi pale inapohitajika kila tunapokutana nanyi Katika vikao mbalimbali,"ameongeza

Amesema kuwa, Tume inawatambua wazalishaji wa maudhui mtandaoni kwa kuwa ni daraja linalowaunganisha na wadau kwa njia ya mawasiliano na wadau muhimu wa Uchaguzi.


Katika muktadha wa Uchaguzi, amesema wazalishaji wa maudhui mtandaoni wana jukumu kubwa la kufanikisha upatikanaji wa habari kwa haraka na kwa wigo mpana Kwa kuelenga makundi ya vijana na watu wanaitumia teknolojia ya kidigitali kwa wingi. 


"Tume inawategemea kuendeshea kampeni za uhamasishaji mitandaoni kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo michoro (art work),video na ujumbe unalenga kuvutia makundi tofauti ya wapiga Kura, hasa vijana na watu wanaotegemea teknolojia kupata habari,"amesema.


Amesema wakati wa kampeni Vyama vya Siasa mutapata fursa ya kuwanadi wagombea na kueleza Sera na Ilani za Vyama vyao,kuwahimiza wananchi kupitia majukwaa yao ya habari kuwa makini na kuhakikisha kuwa hawawi chanzo cha kuvuruga amani na utulivu wa nchi.


"Uzoefu unaonesha kipindi cha kampeni, kunakua na joto la kisiasa linalotokana na baadhi ya watu kukosoa uvumilivu wa kisiasa hali ambayo inaweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi, hakikisheni hamuwi chanzo cha kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu,"amesema.


Ameongeza kuwa, mitandao hasa ya kijamii inekua chanzo muhimu cha habari na elimu kwa kuwa taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao zinapatikana kwa urahisi na kwa haraka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI