Katibu Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Zena Ahmed Said ametoa wito kwa wanawake Viongozi washiriki 70 wa Mafunzo ya Uongozi kutoka katika Taasisi mbalimbali ambao wanashiriki mafunzo ya uongozi ya wiki moja kuwa wasibweteke na majina ama vyeo vyao huku amewataka wawe na wito wa kujiendeleza wakati wote na kwenda kubadilishana uzoefu na watendaji wenzao.
Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar amesema wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika kwa mara ya tatu sasa Katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha na Kuongeza Kuwa Watoto wakike wajiamini Katika nafasi mbalimbali wanazopata hasa kwa kuanzia kwenye familia Zao.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Uongozi Profesa Marcelina Chijoriga amesema kuwa katika mafunzo hayo yanayoshirikisha washiriki kutoka katika Taasisi 19 za serikali huku washiriki wengine wanne wakiwa wamejilipia wenyewe kutokana na utashi wa kujiendeleza wenyewe.
MERCERINA CHIJORIGA Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kwa Mfipa Kibaha amesema
baadhi ya washiriki wa Mafunzo Hayo wamesema wanaimani yatawajengea uwezo katika kazi Zao Pamoja na wale wanaofanyanao kazi kwani wataweza kushirikiana na kubadilishana uzoefu wa kiuongozi.
Mhandisi ANIFA CHINGUMBE-Kaimu Meneja TTCL Kagera ameshukuru kwa Mafunzo ya Uongozi aliyowahi kupata katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere amepanda cheo.
JULIETH LYIMO Kiongozi wa Mtandao wa Wanawake Mkoa amesema
Mbali ya kuwa Shule Uongozi ya Mwalimu Nyerere inatoa mafunzo kwa Vyama na makada wa siasa pia Shule hiyo inatoa mafunzo kwa Taasisi binafsi na hata mtu mmojammoja ambao wanakua wanakidhi vigezo vya kupata huduma .
0 Comments