MFUNGWA aliyetumia miaka mitano kuchomba shimo la siri ili atoroke gerezani nchini Brazil akiamini kuwa mipango yake ilikuwa imesukwa kwa umakini mkubwa, kwa kuchimba shimo hilo( handaki )kwa bidii kwa kipindi kirefu bila kugundulika ajikuta anatokea ndani ya ofisi ya askari wa zamu.
Hata hivyo, baada ya juhudi na mateso ya miaka mitano, alipovunja ardhi akitegemea kuwa huru, alijikuta akiwa si uraiani, bali ndani ya chumba cha walinzi wa gereza.
Makosa ya hesabu au kutokujua vizuri mpangilio wa jengo la gereza hilo yalimgeuzia ndoto ya uhuru kuwa kichekesho cha kushangaza.
Tukio hilo limekuwa gumzo katika vyombo vya habari vya kimataifa, likiwa mfano wa juhudi kubwa zisizozaa matunda.
0 Comments