Na Gift Mongi
Moshi
Mgombea ubunge jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro kupitia chama cha mapinduzi Enock Koola amekabidhiwa fomu ya uteuzi na tume huru ya uchaguzi huku akiahidi kutekeleza mambo aliyoagizwa.
Awali kabla ya kufika katika ofisi za tume alipita katika ofisi chama cha mapinduzi na kukabidhiwa barua ya udhamini ambapo alisema amekabidhiwa jukumu la kuleta maedeleo katika jimbo la Vunjo
Alisema baada ya kumalizika kea uchaguzi ndani ya chama chao jukumu lililopo ni kuvunja makundi na kubaki kuendelea kuwa wamoja.
Ramadhan Mahanyu ni katibu wa CCM wilaya ya Moshi Vijijini ambapo alisema chama hicho kinaenda kushinda kwa kishindo na kuhakisha kuwa rais Dr Samia Suluhu Hassan anashinda kwa kura nyingi
Kwa upande wake Lucas Msele smbaye n msimamizi wa chaguzi wa uchaguzi katika majimbo ya Vunjo na Moshi Vijijini alisema tayari wagombea 19 walikuea wameshajitokeza kuchukua fomu hizo. zoezi linalotajiwa kumalizika agust 27
0 Comments