Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Amechangia Kiasi cha Shilingi Milioni 100 katika usiku wa harambee ya CCM Gala dinner 2025 mara baada ya kuzindua harambee hio katika ukumbi wa mikutano wa mlimani city jijini Dar es salaam
CCM Gala Dinner 2025 ni harambee mahsusi iliyoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi
Kwa ajili ya malengo ya kuwezesha utaratibu wa shughuli zote za kampeni Kuelekea Uchaguzi mkuu oktoba 2025
Malengo ya Kiasi cha pesa kinachotazamiwa kukusanywa kwa ajili ya uratibu wa shughuli za kampeni uchaguzi mkuu ni kiasi cha Tsh Bilioni 100
Utaratibu Wa Kutuma Michango ni Kupitia Mitandao yote ya Simu ambapo
1.Utabonyeza *150*50*1#
2.Utaingiza Control Number C02025
3.Utaweka Kiasi
Kwa watumiaji wa Huduma Za Kibenki utalipia kupitia Account namba 0150001GMMT00 -CRDB Bank
Au Control Number C02025
0 Comments