Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Dkt Oscar Ishengoma Kikoyo amefanikiwa kushinda Kura za maoni kwa kupata Kura 4710
Wakati akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi wa Uchaguzi wilaya ya Muleba Bi Agnes Kasera amesema katika Jimbo la Muleba Kusini Kura zilizotarajiwa kupigwa ni 12381 .
Kura zilizopigwa ni 10962 ambapo Kura halali zilikuwa 10751 na Mshindi wa kwanza ni Dkt Oscar Kikoyo aliyepata Kura 4710 na kufatiwa na Saimon Wenfurebe aliyepata Kura 3448
Wengine walioshiriki katika Uchaguzi huo Jimbo la Muleba Kusini ni Denis Kinubi aliyepata kura 1275 , Abdulmajid Ahmada Kura 549, Modest Burchard 444 na Didas Mtambalike Kura 325
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Muleba Athumani Kahara amesema kuwa Uchaguzi huo umemalizika salama na hawana taarifa yoyote ya tukio la uharifu.
Aidha amewaomba wagombea wote kuwa kitu kimoja kwa sasa na kusubiri maamuzi ya Chama na baada ya hapo kuungana kwa Pamoja kutafuta ushindi wa chama hicho katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi October
0 Comments