MKUU wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, amesema mauaji ya Daudi Bazili (56), mkazi wa Kijiji cha Mabana, hayahusiani na migogoro ya wakulima na wafugaji, bali ni tukio la ulipizaji wa kisasi kufuatia uvunjifu wa amani uliotokea siku moja kabla.
Kwa mujibu wa DC Shaka, taarifa za awali zinaonyesha kuwa vijana wawili wanaodaiwa kuhusika na shambulio hilo walihusishwa na tukio la awali na kuchukuliwa hatua, na kwamba walirudi kwa nia ya kulipiza kisasi.
Marehemu Daudi aliuawa akiwa shambani akilinda mazao yake na alitoka kwenda kunywa maji na kukutana na maswahibu hayo.
Familia yake, pamoja na viongozi wa kijiji cha Mabana, wameomba uchunguzi wa kina na kuimarishwa kwa usalama ili kudhibiti matukio kama hayo.
Baadhi ya watu walihusisha tukio hilo na migogoro ya wafugaji wanaolisha Mifugo yao kwenye mazao ya wakulima.
0 Comments