NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMA MEDIA.
MWANZA.Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepiga marufuku viongozi wake wa kata na matawi kushiriki vikao au shughuli zozote zitakazoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Akizungumza na vyombo vya habari leo, Agosti 9, 2025, Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zacharia Obadi, amesema chama kimepokea taarifa kuwa INEC imewaandikia viongozi wake wa ngazi ya chini barua za mwaliko kushiriki vikao vya maandalizi ya uchaguzi. Amesema msimamo wa chama unabaki kuwa kutoshiriki shughuli zozote za uchaguzi hadi pale marekebisho yatakapofanyika.
“Tunawaelekeza viongozi wetu wasishiriki vikao hivyo kwa kuwa msimamo wa Chadema ni ‘No Reform, No Election’. Hatutashiriki mchakato wowote wa uchaguzi bila marekebisho ya mfumo wa uchaguzi,” amesema Obadi.
0 Comments