Header Ads Widget

WAPIGANAJI WA JIHADI WASHAMBULIA MAENEO YA KIJESHI MALI

Wapiganaji wa kijihadi wameanzisha mfululizo wa mashambulizi kwenye vituo vya kijeshi katika miji mingi nchini Mali - shambulio kubwa la tatu kwa jeshi katika kipindi cha mwezi uliopita.

Jeshi la Mali lilisema lilizima mashambulizi ya Jumanne asubuhi, yanayodaiwa "kuwaua" zaidi ya wanamgambo 80, bila kusema kama kulikuwa na majeruhi wengine.

Hata hivyo, kundi la Jama'at Nusrat al-Islam wal Muslimin (JNIM), lenye uhusiano na al-Qaeda lililokiri kuhusika na mashambulizi hayo, lilisema limedhibiti kambi tatu za jeshi.

Kwa zaidi ya muongo mmoja Mali imekuwa ikikabiliwa na uasi mbaya wa wanajihadi wa Kiislamu, pamoja na mashambulizi kutoka kwa vuguvugu lenye kutaka kujitenga.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI