Header Ads Widget

WAKAZI TANGA WAPATA MATIBABU BURE KUTOKA HOSPITALI YA MUHIMBILI, VODACOM

 

Na MWANDISHI WETU

MATUKIO DAIMA MEDIA, TANGA

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na  Kampuni ya Vodacom imeanza kutoa huduma ya matibabu bila malipo kwa wakazi wa mkoa wa Tanga na maeneo ya jirani.

Huduma hizo zimeanza kutolewa katika viwanja vya  Chuo cha Ualimu Korogwe kuanzia leo Julai 21 hadi 23 2025, baadaye  timu hiyo itahamia mkoani Kilimanjaro. 

Huduma zinazotolewa katika kambi hiyo ni pamoja na uchunguzi na matibabu ya macho, afya ya kinywa na meno, magonjwa ya akina mama na afya ya uzazi, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya afya ya akili, sukari na homoni, huduma za maabara, matumizi sahihi ya dawa pamoja na saratani ikiwemo tezi dume.



Wakazi wameombwa kushiriki huduma hiyo ambayo inatolewa na wataalam wabobezi kwenye fani ya afya.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI