Header Ads Widget

WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA UWT RUFIJI WAKUBALIANA OKTOBA WANATIKI KWA DKT SAMIA

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

RUFIJI.Mwenyekiti wa UWT wilayani Rufiji Rehema Mlawa ameongoza mkutano Mkuu wa jumuiya hiyo na kuongoza upigaji wa kura za maoni za kupata Madiwani wa viti maalum kwa tiketi ya CCM wa Jimbo la Rufiji mkoani Pwani huku akiwataka Wajumbe wa mkutano huo kuchagua viongozi bora na wenye sifa watakao wenye uwezo kutetea ajenda za wanawake katika halmashauri ya Rufiji.

Akifungua mkutano huo Mkuu Rehema  uliofanyika katika ukumbi wa Shule ya Wasichana ya Bibi Titi huko Makao makuu ya Wilaya ya Rufiji Utete na kuratibiwa na Katibu wa UWT wilayani Rufiji Mariam Mugasha ambapo Wajumbe wa mkutano huo walipongeza utekelezaji wa ilani ya CCM uliofanyika katika nyanja mbalimbali wilayani humo.

Aidha Wajumbe hao wamempongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri aliyofanya  ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya hiyo ya Rufiji ikiwemo maendeleo ya sekta ya elimu, afya , Barabara kwa kujenga miundombinu ya barabara zinazopitika muda wote.

Hatahivyo Wajumbe hao wamekubaliana kwa pamoja kutiki Oktoba kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa kumpigia kura nyingi mgombea Urais Dkt Samia kwenye uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.


Awali Kamanda wa Taasisi ya kupambania na Kutokomeza Rushwa  TAKUKURU wilaya ya Rufiji Frederick Msae  aliwataadhalisha Wajumbe wa mkutano huo kuto kuchagua Mgombea waliotoa Rushwa kwani Rushwa ni adui wa haki.

Alisema mgombea aliyetoa rushwa hafai kuwa kiongozi hivyo wasimchague bali wachague kiongozi bora katika kuhudumia Wananchi.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI