Na Lilian Kasenene, Morogoro
Matukio DaimaApp
WAFANYAKAZI wa majumbai wameiomba Serikali kukamilisha mchakato wa kuridhiwa na kupitisha mkataba wa kimataifa wa shirika la kazi duniani (ILO) namba 189 wa kazi zenye staha kwa wafanyakazi wa majumbani kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa haki za msingi za wafanyakazi hao.
Walieleza hayo wakati wa Kikao kazi cha siku mbili cha mafunzo ya utatuzi wa migogoro ya wafanyakazi wa majumbani kilichofanyika mjini Morogoro
Desdelia Saimon, Nasra Seleman ni baadhi yao wafanyakazi wa majumbani ambao wanasema kuchelewa kwa mchakato wa kuridhia mkataba huo kunawafanya waendelee kufanya kazi katika mazingira hatarishi ikiwemo ukosefu wa haki ya faragha na maisha binafsi pamoja na kinga ya kisheria ya kutosha.
“Endapo utaridhiwa utatufungulia mambo mengi sana kwasababu mkataba ule unatuhusu moja kwa moja sisi wafanyakazi wa majumbani, tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuridhia mkataba huu ili na sisi tutendewe haki kama wafanyakazi wengine”, amesema Nasra Selemani, Mfanyakazi wa majumbani kutoka Dar es Salaam.
Zanini Athuman, Mwenyekiti wa wafanyakazi wa majumbani Tanzania, anasema mkataba huo wa ILO unaweka wazi stahiki halali kwa wafanyakazi wa majumbani, ikiwemo kupewa mapumziko ya kutosha, kuishi katika mazingira ya heshima (hasa kwa wanaoishi kwa waajiri), Pamoja na uwepo wa sheria mbalimbali hapa nchini zinazo litambua kundi hilo, bado kuna ugumu katika utekelezaji wake kutokana na sheria kutoruhusu nyumba ya mtu binafsi kuwa ofisi ya kazi. Mwarobaini pekee unaotazamiwa ni kuridhiwa kwa mkataba huo.
Kwa upande wake Katibu mkuu chama cha wafanyakazi wa majumbani, Hifadhini, Mahotelini, Huduma za kijamii na ushauri (CHODAWU) Said Wamba, amesisitizo wafanyakazi wa majumbani kujiunga katika vyama mbalimbali vya wafanyakazi ili kuwa na sauti ya pamoja ya kupambania haki na stahiki zao.
“Tunajaribu kuwainua hawa wafanyakazi wa majumbani wapo chini mno, na hili si jambo la CHODAWU pekee bali jamii nzima ya watanzania inajukumu la kufanya kuwaokoa hawa wafanyakazi wa majumbani kwasababu wanafanya kazi kubwa na muhimu kwa waajiri wao na taifa kwa ujumla lakini hawapati matunda ya jasho lao,”amesema Wamba.
Ili kuhakikisha haki za wafanyakazi wa majumbani zinalindwa ipasavyo, Shirika la kazi Duniani (ILO) limewakutanisha kwa pamoja mkoani Morogoro Tume ya usuruhishi na uamuzi (CMA) Taasisi ya Serikali inayohusika na utatuzi wa migogoro ya kazi Tanzania bara pamoja na wawakirishi wa wafanyakazi wa majumbani katika kikoa kazi cha siku mbili lengo kutafuta mwarobaini wa pamoja wa kukabiliana na changamoto zinazo likumba kundi hilo muhimu katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, mratibu wa mradi wa kuboresha utambuzi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa majumbani kutoka ILO, Chiku Semfuko amesema mafunzo hayo yatawawezesha wafanyakazi wa majumbani kutambua mahali sahihi pakupeleka migogoro yao na kupta utatuzi.
Usekelege Mpulla, Mkurugenzi na Mtendaji mkuu CMA Tanzania bara, Tume imekwisha andaa mwongozo maalumu wa utatuzi wa migogoro ya wafanyakazi kwaajili ya wafanyakazi wa majumbani tu lengo ni kutafsiri utatuzi wa migogro mapoja na kutekeleza matwaka ya kisheria pamoja na mkataba namba 189.
“Tumejipanga kuhakikisha haki za wafanyakazi wa majumbani zinatolewa kwa wakati na mafunzo haya yatakapo kamilika tunaamini wasuruhishi wanao husika na migogoro watapata uwezo wa kumaliza migogoro kwa haraka”, Amesema Mpulla.
Awali Kamishna msaidizi Idara ya kazi Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu Rehema Moyo, mgeni rasmi wa mafunzo hayo amesisitiza CMA kuhakikisha wanatoa kipaumbele kushughulikia migogoro ya wafanyakazi wa majumbani kutokana na ugumu wa mazingira ya kazi wanayopitia kupata stahiki zao.
“Ni muhimu pia hata wenyewe wafanyakazi wa majumbani wajue haki zao pamoja na kuwa vyombo vipo vya kisheria lakini lazima wapewe elimu wa kutambua wapi waende kupata utatuzi wa migogoro yao”
Wafanyakazi majumbani walia na mchakato kuridhiwa, kupitishwa kwa mkataba namba 189.
Summary: Kuridhiwa kwa mkataba namba189 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) ni hatua muhimu ya kuwapa wafanyakazi wa majumbani hadhi, heshima na ulinzi wanaostahili katika mazingira yao ya kazi. ucheleweshaji wa mchakato huo huendelea kuwafanya wafanyakaizi wa majumbani kufanya kazi katika mazingira hatarishi huku wakikosa mikataba rasmi, mapumziko, haki ya faragha na kinga ya kisheria
0 Comments