Header Ads Widget

WADAU WA ELIMU DSM WAPONGEZA CHUO KIKUU MZUMBE KUWASOGEZEA HUDUMA ZA UDAHILI


Wananchi mbalimbali wakiwemo  wanafunzi, wazazi na wadau wa elimu wamefurika katika Banda la Chuo Kikuu Mzumbe lililopo Mlimani City Mall jijini Dar es Salaam ikiwa ni kambi maalumu ya kutoa huduma za udahili kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Huduma hizo zimeanza kutolewa na Chuo hicho kuanzia leo tarehe 13 Julai kwenye kambi zilizowekwa katika mikoa mitano: Dar, es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya. 

Huduma zinazotolewa katika kambi hizo ni utafanuzi wa programu mbalimbali za Chuo Kikuu Mzumbe, sifa na vigezo vya kujiunga na kozi mbalimbali, ushauri wa kitaaluma, na udahili wa papo kwa hapo. 

Akizungumza mara baada ya kupatiwa elimu ya uchaguzi wa kozi, sifa na vigezo Muhitimu wa kidato cha sita Bi.Hosanna Senoline amesema wahitimu wote wanahitaji kupatiwa mwongozo kabla ya kufanya uamuzi wa kujiunga na kozi kwani itawasaidia kufanya maamuzi sahihi ya maisha yao ya kitaaluma kwa utashi wao binafsi

"Wanafunzi wengi hatujui ukisoma kozi gani unakuwa mtaalamu wa kitu gani, bali huwa tunajiunga tu na vyuo kwa kuwa nafasi za kujiunga zipo; hivyo, elimu hii inayotolewa na Chuo kikuu Mzumbe ni muhimu sana kwa wahitimu wa sekondari kuipata kabla ya kufanya maamuzi ya kujiunga na Chuo Kikuu. Hii itatusaidia kujiamulia maisha yetu ya kitaaluma sisi wenyewe. Kwa hiyo, ninatoa rai kwa watu wajitokeze kupata huduma hii hapa Mlimani City hadi tarehe 22 Julai kwani ni fursa adhimu sana". Alisisitiza Hosanna


Katika hatua nyingine, Afisa Uhusiano wa chuo Kikuu Mzumbe, Bi. Fatna Mfalingundi amebainisha kwamba lengo la kuweka kambi katika mikoa mbalimbali ni kuwapa urahisi wa kupata habari kwa wadau wa elimu na wanafunzi watarajiwa wanaotaka kujiunga na Astashahada, Stashahada, Shahada za Awali, Shahada za Umahiri, na Shahada za Uzamivu. 

Afisa Uhusiano huyo ameendelea kuwakaribisha  wakazi wa Dar es Salaam na mikoa jirani kutumia nafasi hiyo kwani  Maafisa mahiri wa Chuo Kikuu Mzumbe wapo kuwahudumia  kila siku kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni na kuongeza hakuna kiingilio na ushauri unatolewa bila malipo



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI