Header Ads Widget

UMRI WA KUNYWA POMBE KUONGEZWA KENYA HADI MIAKA 21

Mamlaka ya Kitaifa ya Kampeni dhidi ya matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya (NACADA) inapanga kutekeleza sheria kali zaidi kuhusu uuzaji na unywaji wa pombe na dawa za kulevya.

Sera ya taifa hilo ya kudhibiti matumizi haramu ya pombe, na dawa za kulevya yam waka 2025 inapendekeza hatua kali ambazo Mamlaka inaamini zitamaliza tatizo la unywaji pombe uliokubuhu nchini, haususan miongoni mwa vijana.

Baadhi ya sheria hizo ni pamoja na kupiga marufuku uuzwaji wa pombe karibu na shule na maeneo ya ibada, huku ikisisitizia marufuku ya unyanyasaji wa pombe wa kupindukia na matumizi ya madawa ya kulevya.

Kadhalika, sera hiyo inalenga kuzuia uuzaji wa pombe kwa watoto walio chini ya chini ya miaka 21 huku pia ikiimarisha ulinzi kwa wale wanaotaka kujiepusha na pombe na dawa za kulevya.

Baraza la Mawaziri liliidhinisha sera hiyo mnamo mwezi wa Juni 24, baada ya serikali ikuiruhusu mamlaka hiyo kutekeleza sheria mpya.

Takwimu ziliripoti kuwa asilimia 87.3 ya wanafunzi hutumia pombe, sigara kwa asilimia 64.4, na shisha kwa asilimia 41.2.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI