Header Ads Widget

UBIA WA SEKTA BINAFSI NA SERIKALI WATAJWA KUWA MSINGI WA MAENDELEO YA TAIFAKWA MIAKA 25 IJAYO.

Na Chausiku Said 

Matukio Daima Mwanza

Katika kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2050, wadau mbalimbali wa maendeleo wanatarajia kukutana jijini Mwanza kujadili nafasi ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi katika kufanikisha malengo ya taifa.

Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Lupa Ramadhani, amesema kongamano hilo litakalofanyika kesho ni hatua ya awali ya utekelezaji wa dira hiyo, likiwa na lengo la kupanua ushiriki wa wananchi na kuhimiza uwajibikaji wa pamoja katika kujenga taifa.

“Wiki iliyopita, Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2050 ilizinduliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo msisitizo mkubwa umewekwa katika nafasi ya ubia. Hili linatokana na malengo ya dira hiyo yanayohimiza ushiriki wa kila Mtanzania katika kuleta maendeleo ya nchi, sambamba na kuzingatia uwazi na utawala bora,” alisema Dkt. Lupa.

Amebainisha kuwa kongamano hilo litakuwa fursa ya kuchambua nafasi ya PPP katika safari ya maendeleo ya taifa, kubaini changamoto na fursa zilizopo, na kujenga mwafaka kuhusu namna ya kuoanisha juhudi hizo na vipaumbele vya dira hiyo, huku ushirikiano wa sekta binafsi na umma ukitajwa kuwa kichocheo kikuu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Habari wa PPP, Chely Matuzya, amesema kongamano hilo lililoandaliwa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi, linatarajiwa kuibua hoja nzito kuhusu mwenendo wa kiuchumi na kisiasa wa taifa katika miongo ijayo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI