Header Ads Widget

TWENDE ZETU KILELENI AWAMU YA TANO YAZINDULIWA RASMI

 


Na Gift Mingi

Moshi

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amezindua rasmi kampeni ya twende zetu kileleni awamu ya tano lengo likiwa ni kuhamasiha utalii wa ndani.

Kampeni hiyo imekuwa ikiratibiwa na kampuni ya Zara Adventure kwa kushirikiana na hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA)pamoja na shirika la hifadhi za taifa (TANAPA).

Babu amesema kampuni hiyo imekuwa ikiratibu kampeni hiyo ambapo kwa mwaka huu litafanyika mwezi desemba mwaka huu.

Alisema jitihada hizo ni kuunga mkono kampeni ya kuutangaza utalii uliokoasisiwa na rais dkt Samia Suluhusu Hassan kupitia filamu ya The royal Tour

Alisema kupitia filamu hiyo watalii wameongezeka tofauti na miaka mingine na kukuza pato la taifa kwa ujumla.




'Kwa mkoa wa Kilimanjaro hotel zinajaa hivyo ipo haja ya kuendelea kujenga hotel kukidhi idadi ya watalii'alisema

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo ya Zara Zainabu Ansell amesemankuwankwa mwaka huu kampuni imeshinda tuzo ya kampuni bora ya utalii kitaifa na kuwa inaleta faraja na na imechangiwa na jitihada zinazoendelea kufanywa

Alisema kwa mwaka huu anatarajia kuwa na wapanda mlima takribani 200 ikihusisha mbalizi wa nchi mbalimbali na waandishi wa habari.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI