Header Ads Widget

SHIRIKA LA INADES FORMATION LAZINDUA KAMPENI MATUMIZI YA MATANDIKO KWA AJILI YA PUNDA

 


Na Thobias Mwanakatwe, Singida

Shirika la INADES Formation Tanzania (IFTz) kwa ufadhili wa Brook East Africa kutoka nchini Kenya limeanzisha kampeni ya matumizi ya matandiko na mikokoteni bora kwa lengo kumsaidia punda asipate michubuko na vidonda anapokuwa amebeba mizigo.

Kampeni hiyo ambayo inaitwa Pakia kwa Kujali ikiwa na kauli mbinu ya Punda ana Thamani Kuliko Mzigo, ilizinduliwa juzi wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu hadi sita ya mradi wa ustawi wa mnyama kazi punda ambayo yalifanyika katika Kijiji cha Kinyamwenda Halmashauri ya Wilaya ya Singida.


Mkuu wa Idara ya Mafunzo kutoka Shirika la INADES Formation Tanzania,Jackline Nicodemas, alisema kampeni hiyo inalenga kupunguza mateso kwa punda yanayotokana na matumizi ya vifaa visivyo bora katika kubeba mizigo pamoja na kutotumia matandiko.

Nicodemas alisema kampeni hiyo itatekelezwa katika vijiji vyote vinavyotekeza mradi wa ustawi wa mnyama kazi punda ambavyo ni Kinyamwenda, Ghata na Endeshi na kwamba ni matumaini wananchi wataipokea kampeni hiyo na kuitekeleza.


Naye Daktari wa Afya na Tiba ya Wanyama kutoka Shirika la INADES Formation Tanzania Dk.Charles Bukula, alisema punda amekuwa akipata vidonda sana anapotumia vifaa ambavyo sio rafiki.

Alisema wananchi wamekuwa wakiwafundisha wananchi namna ya kumtunza punda ili aweze kuwazalishia zaidi na pia wataalam waliopo kwenye vijiji vya mradi wanajengewa uwezo ili wawe na utambuzi kujua kama punda ni mgonjwa na kuweza kumhudumia.

Alisema shirika hilo pia linawajengea uwezo wataalam wanaofanya kazi kwenye maduka ya dawa za mifugo kuhusiana na magonjwa yapi yanaosumbua punda na wanawezaje kuwasaidia.


Kwa upande wake Afisa wa Mradi masuala ya mifugo, George Pharles, alisema mchakato wa kutengeneza sheria ndogo umeanza kwenye viiji vya Endeshi na Ghata ambazo zitasaidia kusimamia ustawi wa mnyama punda ambapo kutakuwa na faini kwa wanaokiuka.

Pharles aliiomba Halmashauri ya Wilaya ya Singida kusaidia kuhamasisha na kusaidia utengenezaji wa sheria hizo katika vijiji vyote vilivyopo katika halmashauri hususani ambavyo vina idadi kubwa ya punda.




 



 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI