Salamu za rambirambi zinaendelea kumiminika kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Nigeria Muhammadu Buhari, ambaye alifariki Jumapili katika kliniki ya London akiwa na umri wa miaka 82.
Jumuiya yakiuchumi ya kikanda ya Afrika Magharibi ECOWAS limeiwasilisha pole kwa serikali na watu wa Nigeria juu ya kifo cha rais huyo wa zamani.
Katika ujumbe wa rambirambi, Rais wa Tume ya ECOWAS Omar Alieu Touray, alisifu urithi wa Buhari, akimtaja kama "mwanasiasa mashuhuri ambaye mchango wake muhimu sana uliendeleza demokrasia na ushirikiano wa kikanda katika Afrika Magharibi na katika bara zima la Afrika."
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema: "Kama Afrika Kusini, tunasimama na taifa la Nigeria katika maombolezo yenu. Rais Buhari aliongoza Nigeria kama mzalendo na bingwa sio tu wa sifa bora za taifa lake wakati wa uongozi wake, lakini wa siku zijazo ambazo zilingojea nchi yake kubwa.
Makamu wa Rais wa zamani wa Nigeria, Atiku Abuja pia Alimuelezea marehemu Buhari kama "mtu ambaye maisha yake yalifafanuliwa na uzalendo usioyumba, nidhamu, na kujitolea kwa maisha yote kwa uhuru na umoja wa taifa letu kubwa."
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO) alikuwa ameomba karibu saa moja mapema kwamba Buhari apone haraka baada ya kujua juu ya hali yake ya kiafya.
Nina huzuni sana," alisema katika tweet.
Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio alielezea kifo cha Buhari kama "hasara mbaya".
Alitoa rambirambi zake kwa familia ya marehemu rais, Rais aliye madarakani Bola Tinubu na watu wa Nigeria.
Aidha mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Youssouf, alisema Buhari atakumbukwa kama kiongozi mwenye kanuni na thabiti ambaye aliitumikia Nigeria kwa heshima na imani.
Kwa upande wake, rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDP), Akinwumi Adesina, alimshukuru Buhari kwa "uongozi, uzalendo na huduma ya kujitolea kwa Nigeria".
Rais wa zamani wa Nigeria, Bw. Goodluck Jonathan amemtaja marehemu Muhammadu Buhari kama kiongozi, ambaye "hakuwa na ubinafsi katika kujitolea kwake kwa wajibu wake na aliitumikia nchi kwa tabia na hisia ya kina ya uzalendo."
Vivyo hivyo, rais wa zamani Olusegun Obasanjo ametangaza kuwa kifo cha Muhammadu Buhari ni hasara kwa Nigeria na sio familia yake tu.
Vile vile, mtawala wa zamani wa kijeshi wa Nigeria, Jenerali Ibrahim Babangida amemwagia sifa marehemu Jenerali Buhari.
0 Comments