Header Ads Widget

RC IRINGA AZITAKA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI KULIPA KODI NA KUSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

 


NA MATUKIO DAIMA APP.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James amezitaka taasisi zote na mashirika yasiyo ya kiserikali kulipa kodi kwa wakati na kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa.

Kheri amesema hayo wakati akizungumza na Taasisi hizo na kusisitiza kuwa licha ya kuweka vipaumbele katika kusaidia na kuhudumia wananchi waweke kipaumbele cha kupambana na rushwa.

Alisema kazi ya kuzuia na kupambana na rushwa ni ya kila mmoja, wasipozuia na kupambana na rushwa watakuwa wamechagua kuwa na nchi isiyokuwa na muelekeo.

"Tutatenga fedha za maendeleo wachache watazitafuna fedha hizo,tutataka kuchagua viongozi wachache watatuchagulia viongozi hao kwa maslah yao. tutataka kuwa na miradi mizuri wachache watainyakuwa na kuifanya chini ya kiwango matokeo yake tutakuwa na taifa lisilo kuwa na muelekeo"alisema.

"Naomba nichukue fursa hii kuziomba taasisi zote kwa maana ya mashirika yasiyo ya kiserikali kama ambavyo tumeweka vipaumbele kusaidia na kuhudumia wananchi tuweke na kipaumbele cha kupambana na rushwa"alisema.

Aidha alisema kuwa watoe ushirikiano wa kutosha kwa taasisi ya kupambana na rushwa pale wanapoona kuna dalili za rushwa au wanapojiridhisha mtu katoa na kupokea rushwa na pale wanapohitajika kwa ushahidi wasaidie ushahidi upatikane ili hao watoaji na wapokeaji waweze kudhibitiwa.

"Kwa mkoa wa Iringa naomba mapambano ya kuzuia na kupambana na rushwa yanayofanywa na TAKUKURU Mkoa wa iringa yaende sambamba na yaungwe mkono na mashirika yote yasiyo ya kiserikali na iwe na mafanikio makubwa".

"Tukifanikiwa kupambana na rushwa tutakuwa na viongozi wazuri, miradi bora, huduma za viwango kwa kuwa hakutakuwa na rushwa iliyopenyakatika taifa letu"alisema .

Akizungumza Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Iringa Victor Swella wakati akiwasilisha mada kwa viongozi wa baraza la Taifa la mashirika yasiyo ya kiserikali(NACONGO) Mkoa wa iringa juu ya udhibiti wa rushwa kwenye uchaguzi alisema kuwa rushwa katika uchaguzi imefanya wananchi wengi kukosa viongozi wenye maadili..

Swilla alisema kuwa wakati huu ambapo nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu wanaowajibu wa kukutana na makundi mbalimbali na kuzungumza nao ikiwa ni pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali,viongozi wa dini,wanahabari na wazee maarufu.

"Uchaguzi sio mara ya kwanza tunakumbuka mwaka jana tulikuwa na chaguzi za serikali za mitaa, na mwaka huu tutakuwa na chaguzi za  Rais ,Ubunge, udiwani "

Alisema kupitia tafiti zao wamekuwa wakiweka mkazo katika maeneo ambayo yaliwafanya wananchi kukosa haki ya kuchagua viongozi wanaowataka waadilifu kutokana na rushwa.

Mwenyekiti wa NACONGO Mkoa wa Iringa, Fidelis Filipatali alisema kuwa elimu ikitolewa katika ngazi ya jamii kwa kuwaelimisha nini vyanzo vya rushwa kutakuwa na mabadiliko makubwa katika nchi yetu.

"sisi kama nacongo tumefarijika kupata mafunzo haya kutoka TAKUKURU elimu hii tutaichukua na lengo likiwa ni kupata viongozi ambao wapo kwa ajili ya jamii na maendeleo"alisema

Lediana Mng'ong'o Mwenyekiti wa NACONGO Wilaya ya Iringa alisema wanaishukuru takukuru kwa kuwapa elimu hiyo na kwa kutambua mashirika yasiyoya kiserikali.

"Madhara ya rushwa ni makubwa hasa kupata viongozi ambao sio waadilifu ambao hawana sifa, na kuna watu wengine wanatumia rushwa kupata miradi na wanaitekeleza vibaya kutokana na rushwa hivyo Nacongo tutaendelea kuelimisha jamii madhara ya rushwa hasa tunapoelekea katika uchaguzi"alisema

MWISHO




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI