Header Ads Widget

RAIS SAMIA ATAJWA SIRI YA USHINDI MWIBA LODGE

NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

Email:matukiodaima4@gmail.com

0754026299

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu ametajwa kuchochea  Ushindi ya Tuzo ya  Tanzania Leading Luxury Tanted Safari Camp  2025  iliyopata Mwiba Lodge iliyopo wilaya ya Meatu, mkoa wa Simiyu katika Tuzo za Utalii Duniani(World Travel Awards)zilizofanyika Jijini Dar es Saalam wiki iliyopita.

Ushindi huu wa kwanza wa kihistoria kwa  mkoa wa Simiyu na Mwiba Lodge  moja ya hoteli za  hadhi ya nyota tano, iliyopo pembezoni mwa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti umepokelewa kwa shangwe na Serikali na Wananchi .

Akizungumza na waandishi wa habari,Mkuu wa wilaya ya Meatu, Fauzia Hamidu Ngatumbura alisema ushindi wa Mwiba Lodge kama kambi bora ya Kitalii ya kifahari nchini Tanzani, umetokana na kazi nzuri ya Rais Samia Suluhu Hassan kufungua fursa za Utalii hata katika maeneo ambayo hayakuwahi kufikiria kuzoa tuzo za Kimataifa.

"Huu ni ushindi wa wananchi wote wa Meatu na mkoa wa Simiyu, kwani maeneo haya miaka ya nyuma hakuna ambaye angetegemea watalii mashuhuri duniani wangeweza kuyafikia ,kufanya utalii na kupumzika"alisema

Mkuu huyo wa Wilaya alisema, Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kufungua fursa katika sekta ya Utalii na ameitangaza vizuri sana Tanzania yote na kufungua fursa kwa wawekezaji hadi sasa maeneo ya pembezoni yanashinda tuzo za Utalii Duniani.


"Tuzo hizi zinatokana na watalii wenyewe duniani kupiga kura, sasa kama wameweza kuipenda hotel ya Mwiba iliyopo wilaya ya Meatu ni faraja kubwa kwetu na tunatoa wito watalii zaidi kutembelea Meatu kwani kuna vivutio vingi vy Utalii"alisema.

Alisema wanapongeza Mwiba Lodge kwa ushindi walioupata katika tuzo za WTO  na wanaamini, mwakani watashinda tuzo kubwa zaidi ili kutangaza wilaya ya Meatu ,mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla.

" Serikali wilaya ya Meatu tutaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji  wote na kuwawekeza mazingira mazuri ya kufanyakazi kwani pia kufanyakwao vizuri kunaongeza mapato ya serikali na kutoa ajira zaidi"alisema

Meneja wa Mwiba Lodge, Saraphina Albin Tengia alisema wamepokea ushindi wao kwa furaha kubwa ushindi ambao pia umetokana na ushirikiano mzuri wa wafanyakazi na jamii ya Meatu.

"Kwa niaba ya kampuni za Mwiba Holding Ltd tumefurahi sana kupokea tuzo hii ambayo inatuhamasisha kufanya vizuri zaidi katika kutoa huduma bora kwa watalii na kwa jamii kwa ujumla"alisema

Alisema kujituma kwa wafanyakazi, kufanyakazi kwa weledi na uaminifu ni miongoni mwa siri za ushindi ikiwepo pia uwekezaji mkubwa uliofanywa katika hotel hiyo iliyopo katika mazingira bora ya asili ikizungukwa na wanyamapori.

Tuzo hizi zimefanyika kwa mara ya kwanza nchini  tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 na kushirika hifadhi za Taifa, sekta za Utalii Duniani na Wawekezaji katika sekta hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Meatu, Afisa Wanyamapori wa wilaya hiyo,Joseline Mpelasoka  alisema Mwiba Lodge walistahili tuzo hiyo,kutokana na kazi nzuri wanazofanya katika wilaya ya Meatu.

Alisema licha ya kutoa huduma za malazi kwa watalii, kampuni hiyo inafanya utalii wa picha katika wilaya hiyo,uhifadhi wa mazingira na wanyamapori lakini pia inatoa huduma mbali mbali kwa wananchi.

"Mwiba wanatoa chakula cha bure mashuleni, wamejenga vituo vya ulinzi wa wanyama wakali, wamejenga vituo vya afya, nyumba za watumishi wa serikali lakini pia wanafadhili masomo watoto wa Meatu"alisema

Alisema kampuni hiyo, chini ya Taasisi ya Friedkin Conservation Fund imewekeza shughuli za utalii na uhifadhi katika maeneo kadhaa katika wilaya hiyo, ambayo kwa sasa inasifika kuwa na idadi kubwa ya wanyamapori, wakiwepo Tembo, Twiga, Simba na wengine.

Hata hivyo, Mpelasoka alisema bado wilaya hiyo, bado ina maeneo mengine kadhaa ya Utalii ambayo yanahitaji uwekezaji na kwa niaba ya Mkurugenzi wake alialika wawekezaji wengine kufika Meatu kuwekeza.


Mwenyekiti wa chama cha Walimu(CWT) wilaya ya Meatu, Otieno Nundu alisema uwekezaji wa Mwiba katika wilaya hiyo, imekuwa na faida kubwa sio kwa utalii tu bali hata sekta nyingine.

Alisema Mwiba wamekuwa wakitoa chakula bure, wakitoa mafunzo yakujitambua watoto mashuleni, wakifadhili wanafunzi katika vyuo mbalimbali lakini wanapanda miti maeneo mbali mbali.

Mwalimu wa shule ya sekondari  Mwanuzi, wilaya ya Meatu, Byera Mwombeki alisema wawekezaji hao, wameweza kufanikiwa kukomesha matukio ya ujangili na uharibifu wa mazingira kutokana na kushirikisha wanafunzi katika uhifadhi.

"Wamekuwa wakitoa mafunzo mashuleni kuhusu utunzwaji mazingira na wanyamapori na wamekuwa wakiwapeleka mamia ya wanafunzi kila mwaka kutembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti ili kujionea faida za uhifadhi"alisema.

Juliana Masanja mkazi wa eneo la Makao, ilipo Mwiba Lodge alisema wanaimani ushindi huo umechangiwa na mahusiano mazuri baina yao na managementi ya hoteli.

"Watalii wakija huku licha ya kukaa katika hoteli hii kufanya utalii katika maeneo ya jamii na kununua vitu vyetu mbali mbali sisi tumekuwa wanufaika wakubwa wa uwekezaji katika eneo hili"alisema.

Katika tuzo hizo mwaka huu Tanzania iliweka rekodi mpya kwa kushinda jumla ya tuzo 27 duniani, serikali ikinyakuwa tuzo 11 zikiwepo na vivutio bora vya Utalii,bodi bora ya Utalii,Nchi bora ya Utalii Afrika wa safari Pamoja na viwanja vya ndege bora vikiwepo ya hifadhi za Taifa.

Sekta binafsi katika tuzo hizo, ilitwaa tuzo 16 kwa mara ya kwanza katika historia ya tuzo hizo kubwa duniani.NANAZ KOFFEKUP IRINGA TAZAMA BOFYA LINK HII

MIDDLEND IN VIEW HOTEL DODOMA

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI