Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 92, ambaye pia ni kiongozi mzee zaidi duniani, ametangaza kugombea kwake uchaguzi wa urais wa Oktoba 12.
Katika taarifa iliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii leo, alihusisha uamuzi wake wa kugombea muongozi wa nane na "simu nyingi na za kusisitiza kutoka mikoa kumi ya nchi yetu na kutoka ughaibuni."
"Mimi ni mgombea wa uchaguzi wa urais wa Oktoba 12," alitangaza.
"Uwe na uhakika kwamba azimio langu la kukuhudumia linalingana na changamoto kubwa zinazotukabili," aliongeza.
Utawala wa karibu miaka 43 wa Paul Biya umekosolewa, huku wengi wakiutaja kugubikwa na ufisadi, ubadhirifu, utawala mbaya, na kushindwa kwa utawala wake kukabiliana na changamoto za usalama.
Ugombea wake katika uchaguzi huo unafuatia talaka ya kisiasa ya hivi majuzi na washirika wakuu kutoka mikoa ya kaskazini, ambao walikuwa muhimu katika kusaidia kupata kura kutoka sehemu ya kimkakati ya nchi katika chaguzi zilizopita.
Ikiwa Bwana Biya ambaye hajawahi kuposhindwa uchaguzi wa urais atapata muhula mwingine wa miaka saba, atakuwa amekosa mwaka mmoja atimize umri wa karne moja mwishoni mwa mamlaka hiyo.
Kabla ya tangazo lake, kulikuwa na wito unaoongezeka kutoka ndani na nje ya Cameroon kumtaka ajiuzulu kando na kutoa nafasi kwa sura mpya katika usukani wa taifa hilo la Afrika ya Kati.
0 Comments